Saida alikuwa mmoja wa characters ambao waliingia AYANA na kuacha alama kubwa. Mwanzoni tulimjua kama mwanamke aliyekuwa na nafasi muhimu katika maisha ya Tyrone na mama wa Asha. Alikuwa strong, mwenye msimamo, na alionyesha wazi kwamba familia yake ilikuwa muhimu kwake.
Kadri story ilivyoendelea, upande mwingine wa Saida ulianza kuonekana. Wivu, hasira na mambo ya nyuma yakaanza kumfanya afanye maamuzi ambayo baadaye yalimletea matatizo makubwa. Relationship yake na Tyrone pia ilianza kuwa na challenges, mpaka mambo yakafika mahali ambapo Saida akaishia jela.
Wengi tuliamini labda jela ingekuwa sehemu ya kumrekebisha Saida na kwamba siku moja angerudi, angeomba msamaha na pengine angeanza upya maisha yake pamoja na Tyrone. Lakini AYANA ilikuwa na surprise nyingine. π’
Baadaye tulipata habari kwamba Saida alikuwa na hali ya kiafya ambayo hakutaka Asha na Tyrone wajue, bali alimwambia Robert pekee. Na hatimaye, Saida akaondoka duniani akiwa bado hajapata nafasi ya kurekebisha kila kitu na familia yake. π€ποΈ
Saida ameondoka AYANA, lakini character yake itaendelea kukumbukwa. Kutoka kuwa mama, mpenzi, mwanamke aliyepambana na hisia zake, mpaka kufika mahali ambapo wivu ulimpeleka mbali sanaβsafari ya Saida ilikuwa moja ya story ambazo Team AYANA hawatasahau. π’π€
Goodbye Saida. You will truly be missed. AYANA will never feel the same without you.





