HII NI KAMA FILAMU YA KWELI!
Vinícius Júnior baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Atlético Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabéu Stadium, alitengeneza tukio la kukumbukwa sana kama filamu.
Miezi michache iliyopita, Diego Simeone (Cholo) alimwambia Vinícius kuwa Florentino Pérez angeweza kumfukuza, na pia akamwonyesha ishara ya kusikiliza jinsi mashabiki wa Real Madrid walivyokuwa wakimzomea.
Lakini katika mechi hii, Vinícius alijibu kwa vitendo alifunga mabao mawili na kuipa ushindi Real Madrid dhidi ya Atlético Madrid ya Simeone. Kwenye style ya kusherehekea ya mabao yake, alirudia ile ishara ya “sikiliza”… safari hii akiwaambia wasikie jinsi mashabiki wa Bernabéu wanavyomshangilia kwa nguvu.






