UPDATES: Becky 1st February

0

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Simazi juu ya simanzi. Imelia ashaambia familia watapanga mazishi na kutakua na imemorial huku Nairobi. Junior alimwambia atampeleka. Imelia aliambia Junior,napia ungependa sana kujua course od death ya Moses but truth be told ni Trisha. Junior alishindwa sana,Trisha how? Acha sasa niwaonyeshe how Trisha was involved kwa hii kifo cha Moses.

Detective Eric,ndio huyu,amekuja kumeet na Trisha kisiri siri,kisha Trisha akaanza kumshika akimwambia thank you. Eric alimwambia walai wewe ni genius wa hii story. Trisha akamwambia usijali,ebu lamba hii elfu mia moja ufurahi for now. Eric akamwambia wah, alafu ju uko single unaonaje twende out for a date now that umenipea pesa? Trisha aliturn off hiyo request,I dont date broke cops🤣🤣🤣

Junior alirudi mtaa na ako na mawazo sana hadi Sanchez akamuuliza,kwani ukona kadem huku ama rada ni gani? Junior akamwambia leo imekua siku mbaya sana,imagine Moses amekufa na Trisha is the suspect,thats one,alafu two,Lexy si mtoto wa James Jabulani. Sanchola ndio alishangaa sana but akaambia Junior,Trisha ni moto wa kuotea mbali,huyo ikifika kwa hizi story,ogopa sana. Junior akamuuliza mbona,unaongea as if kuna kitu unajua chenye mimi sijui? Sanchez anajua kuna uwezekano Trisha aliua Martha but hawana evidence,so anajua kitu anasema.

Its following day,Lexy alikuja kuuliza Moh kama Tito amefika,not yet,hajafika. Lexy akamwambia anataka kufika ghetto kuulizia story za babake. Moh alimwambia anaeza msindi waende wote pia anataka sana kumuona mtaasiz wake huko. Lexy akamwambia na tukifika huko,niulizie kwa Becky kuhusu babangu,ju madhe anaeza nivako.

Huh! Kumbe Trisha alimuita Junior huku kwa Moses hadi ashampikia breko🤣🤣🤣kisha Trisha akaambia Junior,I want to officially ask you to marry me🤣🤣Junior alicheka akamwambia naona akili yako haina akili,lakini Trisha ako serious,akaambia Junior,unakumbuka kuna wakati nilikuambia I will make things right,Iam doing right now. Junior alikataa,akamwambia weeh wewe apana. Trisha alimwambia I love you,unaeza dhani mimi ni drama queen lakini please niko serious,nakupenda. Maskini Junior,utafanyaje?

Kwa Becky wazimu ashafika,Imelia akamwambia madhe,kwanza anamuita kwa jina, akamwambia nataka kujua babangu na useme ako wapi na sijakuja huku kucheka. Haaa,leo hii Lexy amepata kama Imelia wazimu zake ziko top notch,Lexy kaliwekelewa kofi,kisha akaambiwa sikiza, nimekunyamazia sana siku mingi unadhani mimi ni mjinga,kama unataka kujua babako,enda tumia hizo pesa zako kutafuta babako,alah!🤣🤣🤣

Lexy alijam,akataka kupiga mamake lakini Becky yuko hapo,haezi allow kitu kama hiyo ihappen. Moh alimshika Lexy lakini Lexy akamwambia toka nideal na huyu duanzi wenu. Moh alimwambia wee enda acha mimi nideal nao,enda nitaongea na Becky na Imelia. Lexy amejam hadi akapiga kamtungi ka maji teke kaokotwe huko Mbagathi🤣🤣🤣

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Moh alimuomba Imelia asonge kiasi anataka kuongea na Becky private. Moh akaaambia Becky,mimi siko involved kwa hii drama za Lexy,nilikuja tu na yeye ndio nipate time kuongea story za Junior. Becky alimwambia yani wewe unabetray Lexy ndio ufaidike,same way ulibetray madhe just to get what you want,enyewe hujawai change.

Huku ndani,Imelia ashachoka na Lexy,anasema hata heri angeishi akujua Lexy alikufa kuliko kudeal na hii madness ya Lexy.

Huku nje Moh aliambia Becky,kuna ukweli hujai jua,madhe alikubrainwash walai. Becky alimwambia zii,wewe unasema tu same excuse tangu kitambo ama ju father alikua step dad wako? Moh alimwambia zii,madhe alkudanganya,mimi sikubetray madhe,huyo mzee ndio alitake adavantage of me akaniambia nikiambia mtu ataniua,ikabidi niende kuambia madhe but madhe alikataa,but kusema ukweli I was abused kutoka kwa mamangu yeye mwenyewe,angefaa kunisikia anisupport lakini zii na hivyo ndio ilifanya nikachukia madhe na nikaamua kuaibisha familia ndio madhe pia afeel venye mtu hufeel akiwa humiliated. Wueh. Moh ameamua kufunguka sasa.

Lexy na yeye,anashindwa Moh anafanya nini,akiwa hapo,Sanchez akampita tu hata bila salamu.

Kumbe Becky,kwa kumsikiza Moh,aliona enyewe Moh is right,hadi akamwambia siz,njoo nikuhug mtu wetu. Becky na Moh wakahugiana hapo wakilia tu. Moh ameongea hadi akalia. Punde si punde,Imelia akatoka nje akaona Becky na Moh wamehugiana akashindwa haya,hawa washarudiana. Kumbe wakati huo huo,Sanchez ndio pia anafika,Imelia akamuuliza Sanchola,unakuja kuja huku kufanya nini? Moh akaona yeye aende,lakini Sanchez akamwambia zii Moh,kuna kitu nataka kuambia Becky na Imelia na nataka pia ukue hapa. Moh akashtuka,akajua baaasi huyu amekuja kuchoma.

Waliingia ndani, Moh,Imelia,Becky,Sanchez na mimi,kusikia Sanchez ana nini ya kusema. Moh roho mkononi, Sanchez alijieleza akasema kitu naenda kusema leo,ni ukweli na ni ukweli kabisa. Imelia akamwambia wee ongea bwana. Sanchez akaambia Imelia,nasikia unataka kuenda after Trisha kwa kifo cha Moses,Imelia akamuuliza so? Sanchez akamwambia nilikua nakuomba tu uchoree,ju Trisha namjua sana,huyo dem ni wrong number. Imelia alimwambia sikiza,kama unajaribu kutetea Trisha ama amekutuma ukuje unipe story? I will not stop lakini Sanchez alimwambia si hivyo,nakuambia ju Trisha ndio aliua Martha na ni yeye alimpoison.

Moh kuona si yeye ameshtakiwa,alisema I knew,nilijua sana. Lakini Becky akauliza Sanchez,uko sure? Hapo sasa ndio nawarudisha 3 months ago,day after kifo cha Martha,siku ya sherehe ya Lexy. Trisha alikuja akachukua wine akaweka dawa na akapea waiter akamwambia make sure unampea mama wa nyumba na usipee mtu mwingine. Kumbe Sanchez alikua kwa dirisha akaona kila kitu. Hii ni kionjo tu,acha sasa niwapee sababu maalumu ya mbona Sanchez alitaka Moh abaki🤣🤣🤣

Imelia aliuliza Sanchez uko sure hii story ya Martha hujatunga tu? Sanchez akamwambia zii,hii kitu nasema ukweli na huu ukweli ndio wewe hutaki kusikia ju huyu huyu Moh,amekua akikubrainwasha akinidanganishia. Moh akamwambia wee ebu acha uongo. Becky aliambia Sanchez aendelee kuongea. Sanchez aliwaambia sikiza,Lexy hakuanguka ju alikua amelewa,Lexy alianguka ju alisukumwa na huyu Moh,makosa. Imelia na Becky hawakuamini. Moh akajifunza kunyamaza,Imelia akamuuliza did you push my daughter? Moh alikubali,akamwambia ndio,nilimpush Lexy.

Kumbe Junior na yeye,aliona forms za Trisha ni za ukora akataka kuenda lakini Trisha alifunga mlango,huku kwangu huondoki🤣🤣Trisha alikataa kufungua mlango. Junior akamwambia please fungua mlango before I do something bad kwako. Trisha akamwambia relax,unaona Jabulani ashatransfer mali yake kwa jina lake and guess what,iam the next of kin,so mali yoooote imeenda kwa next of kin. Junior alimwambia ni sawa but yafaa nifikirie kwanza. Wueh! Anaitwa Trisha.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *