Jina langu ni Charles, kijana mpambanaji na mkazi wa jijini Dar es Salaam. Kwa muda mrefu, nimekuwa nikifanya kazi kama fundi makenika (professional mechanic), kazi ambayo nimeiheshimu na kuipenda sana. Hata hivyo, siku zote nilikuwa na ndoto kubwa zaidi: kufungua duka langu la kuuza vipuri vya magari (spare parts).Kwa mwaka mzima uliopita, nilijinyima sana. Nilifanya kazi kwa bidii, nikala kwa uchache, na kuweka akiba kila senti niliyopata. Lengo langu lilikuwa moja tu kukusanya mtaji wa kutosha ili niweze kuagiza mzigo wa maana kutoka nje ya nchi.
Baada ya utafiti wa kina, nilifanikiwa kumpata msambazaji (dealer) mwaminifu kutoka nchini China. Mawasiliano yetu yalikuwa mazuri sana. Tulikubaliana bei, na hata alinitumia picha na video za bidhaa zote nilizohitaji. Nilipoona vile vipuri kwenye video, moyo wangu ulijaa furaha isiyo na kifani. Nilijiona kama nimeshavuka mstari wa umaskini; ndoto yangu ilikuwa inatimia. Kilichobaki ilikuwa hatua moja tu: kutuma pesa ili mzigo uanze safari ya kuja Tanzania.
Siku ya tukio, nilibeba pesa zangu zote akiba ya mwaka mzima na kuelekea benki ili kufanya muamala (deposit) kwa yule msambazaji. Nilikuwa na morali ya juu sana. Lakini nilipofika eneo la benki, kitu cha ajabu kilitokea. Ghafla, nilipoteza fahamu. Sikuweza kuelewa nini kilitokea, ni kama nilipigwa na giza nene au “zuga”.Nilipozinduka, nilijikuta nimezungukwa na umati wa watu waliokuwa wakinitazama kwa mshangao.
Nilikuwa nimechanganyikiwa, kichwa kizito, na sikujua nimefika vipi katika hali ile. Jambo la kutisha zaidi ni kwamba niliporaba mifukoni na kwenye begi langu, pesa zote zilikuwa zimetoweka. Machozi yalinilenga. Nguvu ziliisha. Ndoto yangu ya mwaka mzima iliyeyuka ndani ya sekunde chache.
Wakati nikiwa nimepigwa na butwaa, nisijue la kufanya wala pa kuanzia, mwanaume mmoja alijitokeza kutoka kwenye ule umati. Alinisongelea na kuniambia kwa sauti ya chini, “Kijana, inaonekana umeibiwa kwa njia za kishirikina, lakini usikate tamaa.”Yule bwana aliniambia kuwa kuna mtu anaweza kunisaidia kurejesha kile kilichopotea.








