Leo Tuangalie Ufugaji Asili Wa Kuku

LEO TUANGALIE UFUGAJI ASILI
.
Faida za Ufugaji wa Kuku wa Asili:

01: Chakula – nyama ya kuku na mayai hutumika kama chakula muhimu cha wanadamu, chenye protini.

02: Chanzo cha kipato – mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai.

03: Chanzo cha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.

04: Kuku hutumika kwenye shughuli za ndoa kama vile kutoa mahari na pia ni kitoweo muhimu katika sherehe hizo.

05: Gharama nafuu za kuanzisha na kuendesha mradi huu.

06: Ni kitoweo rahisi na chepesi kwa wageni kuliko wanyama wakubwa

READ Also  What We Know About Raila Odinga’s Death

07: Ni kitoweo kisichohitaji hifadhi, hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika.

08: Kuku na mayai hutumika kwa tiba za asili.

09: Jogoo hutumika kama saa anapowika nyakati za alfajiri na majira mengine.

10: Hutuhabarisha iwapo kiumbe kigeni au cha hatari kwa mlio maalum wa kuashiria hatari.

11: Mbolea – kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao na mabwawa ya samaki.

12: Kuendeleza kizazi cha kuku wa asili hapa nchini.

13: Soko lipo la uhakika, ukilinganisha na kuku wa kisasa kwani nyama na mayai yake hupendwa zaidi na walaji.

READ Also  Here Is The New Update From IEBC

14: Manyoya ya kuku hutumika kama mapambo, pia huweza kutumiaka kutengenezea mito ya kulalia na kukalia.

15: Shughuli za utafiti – kuku wanatumika katika tafiti nyingi za baiolojia, kama kutambua mambo ya lishe. Shughuli za viwandani: • • •

16: Mayai yenye mbegu ya jogoo hutumika katika kutengeneza dawa za chanjo.

17: Magamba ya mayai yanaweza kutumika katika utengenezaji wa vyakula vya wanyama.

18: Kiini cha njano cha mayai kinaweza kutumika kutengeneza mafuta ya kuoshea nywele (shampoo)..
Mapungufu ya Kuku wa Asili:

01: Hutaga mayai madogo wastani wa gm 47 ambapo kuku wa kisasa wastani wa gm 55,

READ Also  The U.S.government Sanctions Tanzania's Police Force Senior Assistant Commissioner Faustine Mafwele

02: aidha hutaga mayai machache wastani wa mayai 60 kwa mwaka ambapo kuku wa kisasa huweza kutaga hadi mayai 250 kwa mwaka. Ukuaji taratibu

03 kuku wa asili hukua taratibu kutokana na lishe duni. huchukua muda mrefu miezi sita) kufikia uzito wa kuchinjwa (kilo 1-1.5 Hali hii pia hufanya faida ya ufugaji wa kuku wa asili kuchukua muda Mrefu. Nyama yake ni ngumu (huchukua muda mrefu kuiva) ikilinganishwa up na kuku wa kisasa

Kwa Ushauri ZAIDI piga 0768876692

Milton

Professional IT expert and experienced news writer/ online marketing expert

Related Posts

Why Mt Kenya People Should Stop Demonstrating

Watu wa Mt kenya cease yourself from holding demos because of finance bill. You are not the only ones who are suffering and will suffer because implications of finance bill.…

Read more

Update: Njugush And Wakavinye Are Allegedly Back Together

Njugush and Wakavinye are allegedly back like they never left. The “juu ya watoto” situation has brought them together again.Acha warudiane, it was just a slight mistake. Sisi kama certified…

Read more

You Missed

Why Mt Kenya People Should Stop Demonstrating

  • By Milton
  • May 25, 2026
  • 3 views
Why Mt Kenya People Should Stop Demonstrating

Update: Njugush And Wakavinye Are Allegedly Back Together

  • By Milton
  • May 25, 2026
  • 4 views
Update: Njugush And Wakavinye Are Allegedly Back Together

Football Titbits Across The Papers

  • By Milton
  • May 25, 2026
  • 4 views
Football Titbits Across The Papers

New Harambee Stars Player Shares This

  • By Milton
  • May 23, 2026
  • 2 views
New Harambee Stars Player Shares This

Jamie Carragher on Arne Slot and the criticism around Arsenal winning the league

  • By Milton
  • May 23, 2026
  • 3 views
Jamie Carragher on Arne Slot and the criticism around Arsenal winning the league

PUBG Mobile & Infinity Ignite Kenya Varsity Showdown With $1,000 Prize Pool And 10 GT 30 Pro Smartphones

  • By Milton
  • May 23, 2026
  • 9 views
PUBG Mobile & Infinity Ignite Kenya Varsity Showdown With $1,000 Prize Pool And 10 GT 30 Pro Smartphones