Taarifa ya uongozi wake inasema “Tumepokea jumbe nyingi za rambirambi kufuatia taarifa zilizosambazwa na klabu ya soka kuhusu kifo cha mtoto aliyedhaniwa kuwa ni mwana wa Aziz Ki.
Tungependa kutoa ufafanuzi kwa heshima kwamba mtoto aliyefariki hakuwa mwana wa Aziz Ki.
Marehemu alikuwa ni mwana wa dada yake Aziz Ki, ambaye kwa masikitiko makubwa alifariki nchini Burkina Faso, akiwa shambani.
Tunashukuru kwa dhati upendo, dua, na rambirambi zilizoonyeshwa na mashabiki, vilabu, na jamii ya soka kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu. Msaada wenu unatambuliwa na kuthaminiwa sana.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, na awape familia nguvu na faraja.
UONGOZI WA AZIZ KI,”





