Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló Apinduliwa

Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló amepinduliwa. Rais Umaro ameripotiwa kukamatwa na maafisa wa kijeshi baada ya milio ya risasi kusikika katika mji mkuu, Bissau kwa siku 3 mfululizo. Shirika la habari la BBC limeripoti kwamba Rais huyo ametiwa mbaroni na maafisa wa kijeshi na kwa sasa yupo chini ya ulinzi.

Brigedia Jenerali Denis N’Canha, mkuu wa Brigedi ya kijeshi mjini Bisau amehutubia kupitia televisheni ya taifa na kutangaza kuwa jeshi limechukua madaraka. Jenerali N’Canha amesema askari wote wa kikosi cha ulinzi cha Rais wamekamatwa pamoja na mawaziri kadhaa.

Kabla ya Jeshi kutangaza mapinduzi hayo, Rais Sissoco alipiga simu kwenye kituo cha televisheni cha France 24 kilichopo Ufaransa kwa sauti ya kutetemeka na kusema: “Nimewekwa chini ya ulinzi, nimeondolewa madarakani” kabla ya simu hiyo kukatwa ghafla.

READ Also  After catching my wife cheating, I never thought forgiveness could bring peace like this again

Guinea-Bissau ilikuwa ikisubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili, ambapo mgombea mkuu wa upinzani Fernando Dias alienguliwa katika orodha ya wagombea ili kumfanya Rais Umaro ashinde kirahisi.

Jenerali N’Canha ametangaza kufutilia mbali matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyoonyesha kumpa ushindi Rais Umaro kwa zaidi ya 90% na amesema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu mkubwa. Jenerali N’Canha ametangaza kufunga mipaka ya nchi, huku akiwataka wananchi wabaki watulivu. Pia ameeleza kuwa Jeshi litaongoza nchi hiyo kwa muda mfupi ili kurejesha hali ya utulivu kabla ya kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

Rais Umaro alikuwa Rais wa kwanza Afrika kumpongeza Rais Samia baada ya matokeo ya uchaguzi wa Tanzania kutangazwa. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter (X) Rais Umaro alipost picha akiwa na Rais Samia na kuandika maneno yafuatayo: “Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Samia Suluhu kwa kuchaguliwa tena. Ushindi huu ni ushahidi wa imani ambayo wananchi wa Tanzania wamempa na ni kielelezo cha dhamira yake thabiti ya kuendeleza na kustawisha Tanzania.”

READ Also  Today's Premier League matches

Nini maoni yako??

  • Milton

    Professional IT expert and experienced news writer/ online marketing expert

    Related Posts

    • MiltonMilton
    • News
    • November 27, 2025
    • 1 views
    • 1 minute Read
    His Old Face Will Never Come Back Again

    In 2021, U.S. Army veteran Randy Adams was seriously injured during an unexpected altercation while on leave in Chicago. What followed was a long, difficult recovery: a month in a…

    Read more

    Vincent Kompany: “Every Team Can Lose, That’s Football”

    Vincent Kompany: “Every team can lose, that’s football. I thought we didn’t have a bad start in the first half, but then conceded from a set piece. Even so, we…

    Read more

    You Missed

    Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló Apinduliwa

    • By Milton
    • November 27, 2025
    • 2 views
    Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló Apinduliwa

    His Old Face Will Never Come Back Again

    • By Milton
    • November 27, 2025
    • 1 views
    His Old Face Will Never Come Back Again

    Vincent Kompany: “Every Team Can Lose, That’s Football”

    • By Milton
    • November 27, 2025
    • 2 views
    Vincent Kompany: “Every Team Can Lose, That’s Football”

    Police Arrest Notorious Burglary Suspects And Recover Stolen Items In Kisumu

    • By Milton
    • November 26, 2025
    • 3 views
    Police Arrest Notorious Burglary Suspects And Recover Stolen Items In Kisumu

    𝐔𝐄𝐅𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐏𝐈𝐎𝐍𝐒 𝐋𝐄𝐀𝐆𝐔𝐄 𝐑𝐄𝐒𝐔𝐋𝐓𝐒

    • By Milton
    • November 26, 2025
    • 6 views
    𝐔𝐄𝐅𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐏𝐈𝐎𝐍𝐒 𝐋𝐄𝐀𝐆𝐔𝐄 𝐑𝐄𝐒𝐔𝐋𝐓𝐒

    Today’s UEFA Champions League Matches

    • By Milton
    • November 25, 2025
    • 7 views
    Today’s UEFA Champions League Matches