Mfugaji fahamu ya kwamba bila kuku wako kulishwa chakula bora na kupewa maji safi na salama yasiyokuwa moto na yanayopatikana muda wote, usitegemee kupata mayai mengi wala nyama nyingiβ¦.
Ulishaji bora wa kuku unapaswa kuanzia kuku akiwa bado kifaranga wa siku moja hadi kipindi chote cha utagaji wake au ukuaji wake kwa wale wanaofugwa kwa ajili ya kuuzwa.
FAIDA YA CHAKULA BORA KWA KUKU:
πKuku hukua haraka.
πKuku hukomaa mapema.
πKuku huwa na afya nzuri.
πKuku hutaga mayai mengi, makubwa na yenye makaka magumu.
πUtagaji huendelea kwa kipindi kirefu.
πNyama huwa nyingi, laini na nyeupe.
πUzito wa kuku huongezeka.






