Mfugaji fahamu ya kwamba bila kuku wako kulishwa chakula bora na kupewa maji safi na salama yasiyokuwa moto na yanayopatikana muda wote, usitegemee kupata mayai mengi wala nyama nyingi….
Ulishaji bora wa kuku unapaswa kuanzia kuku akiwa bado kifaranga wa siku moja hadi kipindi chote cha utagaji wake au ukuaji wake kwa wale wanaofugwa kwa ajili ya kuuzwa.
FAIDA YA CHAKULA BORA KWA KUKU:
👉Kuku hukua haraka.
👉Kuku hukomaa mapema.
👉Kuku huwa na afya nzuri.
👉Kuku hutaga mayai mengi, makubwa na yenye makaka magumu.
👉Utagaji huendelea kwa kipindi kirefu.
👉Nyama huwa nyingi, laini na nyeupe.
👉Uzito wa kuku huongezeka.






