Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hususani Ofisi ya DPP kuchuja makosa ya Vijana walioshtakiwa kwa makosa ya uhaini kufuatia maandamano ya October 29,2025 na kwa wale waliofanya makosa kwa kufuata mkumbo waachiwe huru.
Akihutubia Bunge leo November 14,2025, Dkt. Samia amesema “Natambua kuna Vijana wengi wamekamatwa kwa kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya na wengine wamefuata mkumbo, nikiwa kama Mama navielekeza vyombo vya kisheria kuangalia makosa yaliyofanywa na Vijana wetu, kwa wale ambao walifanya mambo kwa kufuata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu wawafutie makosa yao”
“Ukiangalia clip zile za maandamano unaona kabisa kuna Vijana waliingia kwa kufuta mkumbo, wanaimba kwa ushabiki, naelekeza Ofisi ya DPP kuchuja viwango vya makosa na kwa waliofuata mkumbo wawaachie waende kwa Wazazi wao”





