Hello! Kindly ukiona hii Updates, just do me a favour by downloading M News. The more we download the more we get updates.
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Jojo ndio kanarudi home na mamake akamwambia wakae hapo waongee kiasi..akamuuliza,wewe na madam Salome mnajuana aje? Jojo akamwambia nimemjua juzi tu,ama alikuambia kila kitu? Neema akwamambia yeah,she told me and please achana na issue za wenyewe,this is a very sensitive matter. Jojo akamwambia its ok mum,thanks!
Jojo alikua na good news,akaambia madhe guess what,nimeenda shule kupewa living certificate na nikamconvince wakanipea fee tulikua tumelipa mbele. Mind you,Eddy kabla hajamrufe,alikua amelipa pesa mob sana na sasa washarefundiwa. That was good news.
Lakini sasa, wacha Jojo aangalia Kwa bag,apate hakuna sneakers zake…ziko wapi? Kale kadem kenye hutaka Brayo,kalishaiba😂😂😂
Baraza anapoa poa hadi asharudi nyumbani. Jayden alikuja hapo akamletea kahawa na akauliza babake,kuliendaje ukapata heart attack? Baraza akadanganya,akasema unajua mambo ya uzee but usijali,nitakua sawa. Jayden,deep down anajua mamake alikua huko na mzae…Baraza pia ashajua Jayden alienda kuona mamake but hajawai mwambia.
Baraza alimuuliza Jayden,unakaa wa mawazo sana,mbona? Jayden akamsema nafikiria chenye kilikufanyikia kisirudie tena. Jayden anajua babake alikua na mamake,na Baraza anajua Jayden alikua na mamake shida ni hawataki mmoja ajue anajua😂😂😂
Tufike kwa Salome nyumbani,ndio hata anafika pia. Mzee wake alimwambia naondoka sai, you need anything? Mzee alimwambia leo niko very busy na sitaki unicheleweshe,tunaenda out na mabeshte zangu..Salome alimwambia its ok,leo nilikutana na Jayden,yule kijana wangu mwenye alipotea. Francis alijam,akamuuliza,si tulielewana tuachane na mambo ya umaskini ukuje nikuonyesha utajiri? Just imagine, Francis aliambia Salome, sitaki uniaibishe kwa marafiki wangu wakijua unangea na huyo kijana maskini,alah! Usiniambie hayo mambo yako wewe,shame on you. Wueh! Salome,atafanya nini sasa ju aliambia Francis awe in boy’s life but Francis hataki kusikia any of such nonsense.
Francis akamwambia naona ushaamua kureunite na mtoto wako,acha sasa nikusaidie, I will file for a divorce na nikuachilie utoke uende ukae na mtoto wako na ujue utaenda venye ulikuja, hakuna mali utaenda nayo kutoka hapa kwangu!
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Its evening, Neema alikuja kukaa hapo nje kupunga kahewa kiasi. Kumbe Sharon alimuona akakuja akamuuliza kwa giza unafanya nini,ama unataka kusema imekua mbaya? Neema akamuuliza nini hiyo? Sharon akamwambia niliona Rachael akitoka huku morning but usijali,huyo hatakueza kwa urembo.
Huh! Sharon akiwa hapo,Mark akafika akawasalimia tu vizuri “habari zenu” Sharon akamwambia hutaziweza,mbona unaonyesha Neema madharau after Rachael amekuja huku? Huoni venye Neema ni mrembo amekuzalia watoto watatu? Sharon huwa anadhani Neema ni bibi wa Mark na akina Cate ni watoto wake😂😂😂Mark aliambia Sharon please, enda kwako sasa hivi.
Sharon alijibeba akaenda kisha Mark kuambia Neema kama wanaeza ongea,Neema alikataa akamwambia ni late sana na nataka kuenda kulala.
Richard pia alikuja akaambia Naomi,ameongea na Eddy kwa simu..akauliza Naomi,kumbe wewe ndio ulihook up Eddy na Karen. Naomi akamuuliza unamaanisha nini? Richard akamwambia,wewe hata sikujui sasa,sijui wewe ni mwanamke wa aina gani,I wish divorce iishe haraka nihame,wewe siezi taka kukaa na wewe hata siku moja.
Rachael alikuja akakutana na mamake na kuulizwa kuhusu watoto na bwanake? Rachael akamwambia watoto wako sawa na baba yao ako tu! Kisha Rachael akamwambia,guess what mum,nimekutana na Mark na hata ako handsome tu kama kitambo…mamake akamuuliza tu swali moja
“umemwambia ile kitu”
Rachael akamwambia apana mum,nitaanzaje? Mamake akamwambia wewe ushakua mtu mzima hufai kuendelea kumficha,sai yafaa uwe ushamwambia akae akijua.
Kwani ni nini Rachael yafaa aambie Mark? Tutakuja kujua!
Barua kutoka jela. Eddy kuna barua aliandikia Neema akimuomba msamaha na kusema anajuta sana kwa Neema kuja kumuona akiwa na huyo boyfriend wake. Kwa Barua,Eddy anauliza Neema,yani 6 months already ushapata replacement yangu😂😂😂amesahau yeye hata siku mbili hazikuisha alikua ashapata replacement ya Neema,sai kusikia tu fununu ati Neema ako na Mark,inafanya mwanaume anaandika barua😂😂😂
Siku iliyofuata, Mark wakienda kazini, Alphose alikuja hapo akaona Neema ako little bale, akamuuliza kama ako sawa? Neema akamwambia niko sawa. Sharon pia alikua hapo,akauliza Alphonse,mamako alinipenda nasikia alikuja kuniona? Alphonse akamwambia sikuelewi unaongelea nini…Sharon hakunyamaza,akamwambia tukiwa wawili tutaongea but ujue ukinioa sitakaa na huyo mamako😂😂Alphonse akashindwa,rada ni gani na huyu Sharon but anaelewa ni wazimu nusu.
Kumbe ile barua, Eddy kupea lawyer wake atumie Neema,lawyer na yeye,badala ya kutumana barua,akakuja nayo kwa Karen😂😂😂akamwambia sikiza, niko na barua ya Neema hapa kutoka kwa Eddy na sasa nina shida ya 10k nahitaji sai,so 10k for the letter…Ilibidi Karen apeane 10k just to get hold of that letter,so barua,haikumfikia Neema,😂😂😂
Sikuhizi fb wako na mimi so kindly,iam requesting,for online cyber services number iko hapo kwa bio,get in touch anytime.
Leave a Reply