
House girl alitandika kitanda cha boss wake kama moja ya majukumu yake, Alipomaliza akakitazama kisha akasema
“nisije nikafa bure bila kukilalia kitanda hiki” akavua nguo zake akabaki na chupi akawasha AC akapanda kitandani akajifunika blanketi akalala, usingizi ukampitia akalala fofofo.
Mume wa boss wake akarudi nyumbani mapema siku hiyo japo sio kawaida yake, alipoingia chumbani akakuta kuna mtu kalala, akajua ni mkewe maana wamekorofishana usiku wa kumkia siku hiyo hivyo akajua bado anahasira.
Mume akavua nguo zake akabaki na boxer akalifunua blanket taratibu ili aliyelala asimsikie akajifunika akalala akasinzia fofofo.
Boss akarudi yaani mke akakuta watu wawili wamelala… Akawafunua haraka kisha akawaamsha.
CHEMSHA BONGO:
- Je, wewe ndio ungekuwa yule boss/mke ungewaelewa?
- Kama wewe ndie ungekuwa mume wa yule boss ungejitetea vipi?
- Kama wewe ungekuwa yule mfanyakazi ungejitetea vipi??
- Hiyo yote imesababishwa na nani? Mke/boss, mume au mfanyakazi
Leave a Reply