TAWA YAMDHIBITI MAMBA ALIYEZUA TAHARUKI BUCHOSA

  • MilMil
  • News
  • October 4, 2024
  • 0 Comments

Kijiji cha Kahunda charindima Kwa nderemo na vifijo

Na. Beatus Maganja

Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini – TAWA kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Kahunda kilichopo Kata ya Katwe Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema na mkoa wa Mwanza wamefanikiwa kumdhibiti mamba aliyezua taharuki takribani wiki nzima Kijijini humo kabla ya kuleta madhara Kwa binadamu.

Tukio la kumdhibiti mnyama huyo mkali na mharibifu lilitokea oktoba 03, 2024 mara baada ya wananchi wa Kijiji hicho kutoa taarifa kwa Maofisa wa TAWA Kanda ya ziwa kituo kidogo cha Mwanza ambao walifika haraka eneo la tukio na kufanikiwa kumdhibiti mnyama huyo Kwa kumuua Kwa mujibu wa Sheria.

READ More  Update: Here Is Auditor General's Report About Misuse Of NG-CDF Funds By MPs
Ad 2
Ads: Click image 👆 & Download M News

Wananchi wa Kahunda wamesema mamba huyo amekuwa akileta taharuki takribani wiki nzima Kwa kukamata mifugo yao wakiwemo bata, kuku na mbwa Katika mwalo wa Kijiji hicho na Kijiji cha zabaga hali ambayo ilikuwa ikiwafanya waishi Kwa wasiwasi mkubwa na kushindwa kufanya shughuli za kibinadamu Kwa amani katika ziwa hilo.

READ More  President Ruto, Raila Odinga In Addis Ababa Ahead Of AU Election

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kahunda Bw. Athumani Wambura ameipongeza Serikali kupitia maofisa wa TAWA kwa kufanikisha zoezi la kumdhibiti mamba huyo na jitihada zote zinazofanywa na taasisi hiyo Kijijini humo ikiwa ni pamoja na hatua mbalimbali wanazochukua Katika kulinda maisha ya wananchi wa wilaya ya Sengerema dhidi ya athari za wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko.

READ More  US Election: What You Should Know

“Niseme tu nawapongezeni sana hawa ndugu zangu wa maliasili (TAWA) jambo walilolifanya ni kubwa kwa wananchi wetu, Kwa namna moja au nyingine tumepata amani kwa kumdhibiti huyu mnyama ambaye ni tishio kubwa sana. Kwa miaka ya hivi karibuni wanyama hawa wameweza kuua watu wetu zaidi ya watatu katika Kijiji cha Kahunda” amesema
Athumani Wambura. Continue reading.

Mil

Related Posts

Today’s Fixtures

ENGLAND: Premier League 14:30 Manchester City vs Everton17:00 Bournemouth vs Crystal Palace17:00 Chelsea vs Fulham17:00 Newcastle vs Aston Villa17:00 Nottingham vs Tottenham17:00 Southampton vs West Ham19:30 Wolves vs Manchester Utd22:00…

Read more

The 10 Things To Do At The Age Of 25 Years

Take care of yourself with love and kindness. Have a nice weekend and see you soon. Share this… Ads: Click image 👆 & Download M News Facebook 0 Pinterest 0…

Read more

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Today’s Fixtures

  • By Mil
  • December 26, 2024
  • 2 views
Today’s Fixtures

The 10 Things To Do At The Age Of 25 Years

  • By Mil
  • December 25, 2024
  • 7 views
The 10 Things To Do At The Age Of 25 Years

Why Oscar Sudi Is In Trouble With His Degree

  • By Mil
  • December 24, 2024
  • 11 views
Why Oscar Sudi Is In Trouble With His Degree

Football Titbits across the papers

  • By Mil
  • December 24, 2024
  • 7 views
Football Titbits across the papers

Today’s Premier League Fixtures

  • By Mil
  • December 22, 2024
  • 25 views
Today’s Premier League Fixtures

Sad Update: Ezekiel Otuoma is dead

  • By Mil
  • December 21, 2024
  • 38 views
Sad Update: Ezekiel Otuoma is dead