Kesi hiyo imeahirishwa baada ya Mshitakiwa Tundu Lissu kuweka pingamizi dhidi ya upande wa Jamhuri kwa shahidi wa nne wa siri (Witness chamber) atokee kizimbani kwani Shahidi huyo kutoa ushahidi wa siri si salama kwake kama mshitakiwa.
Katika pingamizi Hilo,Lissu alichukua muda wa masaa mawili kutoa kanuni sita zinazokataza shahidi wa siri ikiwemo kanuni za ulinzi wa mashahidi za mwaka 2025, ambapo amesema kiboski ambacho shahidi yupo ni kizimba maalum cha ushahidi ambacho hata majaji hawatamuona katika kutoa ushahidi au kumuona isipokuwa mawakili pekee wa Serikali.
Baada ya pingamizi hilo upande wa Jamhuri kupitia kwa Nassoro Katuga umesema hoja za mshitakiwa zilikuwa nyingi na kuomba majaji na Mshitakiwa wawape muda wa kupitia kanuni hizo,ombi ambalo lilikubaliwa na Mshitakiwa Tundu Lissu na majaji. #EastAfricaTV





